Diamond Afungukia Hatma Ya Wasafi Festival

Msanii wa muziki wa Bongo fleva na CEO wa WCB Diamond Platnumz amefunguka na kuzungumzia mipango ya Wasafi Festival mara Baada ya kuachwa huru na BASATA.

Katika mazungumzo yake na Waandishi wa habari siku ya leo, Diamond amewataka mashabiki zake waendelee kuwa wavumilivu  kuhusu tamasha lao la Wasafi Festival kwani bado wanafikiria kama walianzishe upya au waendelee kufanya shoo mikoa iliyobakia, lakini kwakuwa tayari wameshafunguliwa basi hakuna shaka juu ya hilo watawajulisha kitachoendelea.

download latest music    

Namshukuru  mwenyezi Mungu kwakuniweka hai na salama mpaka nafika hapa, lakini pia kabla yakuanza chochote pia niishukuru serikali yangu pendwa kwakunifungulia kifungo ambacho nilikuwa nacho, maana kifungo kinafunguliwa tu na neema hizo zinakuja.

Niwashukuru watu wote ambao wameisapoti Wasafi Festival, nawashukuru sana kwa sababu mapokezi yalikuwa makubwa hatukuyategemea, lakini mimi na menejimenti yangu tulikuwa tunajadili tumalizie ile mikoa iliyobaki au tuanze na upya mwaka 2019, japo mzani unaelemea mwaka 2019 ili watu waliokuwa bado hususani mikoa ambayo hatujenda wawe na hamasa zaidi, hivyo tunawaomba mashabiki zetu wasichoke kutusapoti na kuendelea kuzifatilia kazi zetu nzuri“.

Diamond na Rayvanny walifungiwa na BASATA mwishoni mwa mwaka jana baada ya ku-perform wimbo wao wa Mwanza Nyegezi kwenye Tamasha lao la Wasafi Festival jijini Mwanza, wimbo ambao umefungiwa na Baraza hilo. Lakini juzi Baraza hilo lilitangaza kuwafungulia baada ya kuomba radhi.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.