Diamond Amekataa Kumpa Hamisa Milioni Tano Kila Mwezi Kwaajili Ya Malezi Ya Mtoto

Mwanamuziki Diamond Platnumz amekuwa kwenye mgogoro na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto tangu Hamisa alipovujisha picha zao za faragha na kupelekea Diamond kukiri kuwa amezaa na Hamisa.

Baada ya sekeseke hilo kutokea Diamond alikata mawasiliano na Hamisa na kuacha kumuona mtoto wake huku Hamisa akidai kuwa Diamond aliacha kabisa kulea mtoto na hakuwahi kutoa hela ya matumizi kitendo kilichopelekea Hamisa kumfungulia Diamond kesi ya madai ya kumtelekeza mtoto na kudai alipwe shilingi milioni tano kwa mwezi kutokana na kipato kikubwa cha Diamond.

download latest music    

Baada ya kupokea tuhuma hizo Diamond aliiambia mahakama kuwa hana uwezo wa kumlipa Hamisa milioni tano kwa mwezi Kama gharama ya kumtunza mtoto. Diamond amewasilisha majibu hayo katika mahakama ya watoto Kisutu, mbele ya hakimu mkazi Devotha Kisoka baada ya Mobetto kumfungulia kesi hiyo mwezi uliopita.

Katika majibu yake, Diamond amedai fedha hizo anazodai Hamisa alipwe kwa mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto ni kubwa na hawezi kuzimudu. Hamisa katika maombi yake kupitia kwa mawakili wake Abdullah Lyana na Walter Goodluck wa kampuni ya uwakili ya Century attorneys, anaiomba mahakama imwamuru Diamond, kutoa matunzo ya mtoto kila mwezi, mtoto huyo wa kiume aliyezaa na msanii huyo na kumuomba msamaha kwa umma kwa madhara yaliyoishtua familia yake.

Baada ya kupokea majibu hayo mahakama ilihairisha kesi hiyo ya madai hadi Novemba 8, Mobetto kwa kupitia wakili wake walimpa notisi Diamond ya kutaka amwombe radhi na kupeleka matunzo ya motto ndani ya siku saba lakini notisi hiyo haikutekelezwa hivyo wakapeleka kesi yao mahakamani.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.