Diamond amenunua helikopta?

Uvumi umezuka mtandaoni kuwa Diamond Platnumz sasa ni mmiliki wa helicopther ya aina AgustaWestland A109S inayo gharimu TZS bilioni 14.5.

Baadhi za vyombo vya habari vilianza kusambaza habari hii baada ya Diamond kuonekana amepiga picha akisimama mbele ya helikopta hio.

download latest music    

Ukweli wa mambo ni kuwa ndege hio inamilikiwa na Akagera Aviation – kampuni ya ndege ya aina ya helikopta ambayo iko jijini Kigali.

Diamond alibebwa na ndege hilo linalomilikiwa na Akagera Aviation baada ya kufika nchini Rwanda. Baba Tiffah alikua anatoka Kongo ambapo alitumbuiza mashabiki jijini Goma.

Tazama video hapo chini uone jinsi Diamond aliingia Rwanda akitoka Kongo:

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere