Diamond Amuomba Mama yake Kuwapenda Wajukuu Wote,

Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Diamond Platinumz amefunguka na kumuomba mama yake kuwapenda wajukuu zake wote bila kuwabagua kama vile ambavyo amekuwa akimpenda yeye.Diamond ambae kila siku amekuwa muwazi kwa kila wanachofanya ndugu zake hakusita kuyasema hayo katika siku ya kuzaliwa ya mama yake.

Akiandika ujumbe mzito wenye kumtakia kheri ya sikukuu ya kuzaliwa mama yake mpenzi, Diamond pamoja na kumshukuru na kumuhaidi vitu vingi lakini hakusita kusema kuwa kama vile ambavyo anajua mama yake amekuwa akimpenda sana na anajua bado anampend basi pia awapende wajukuu zake wote bila kuchagua yupi wa kumpenda zaidi kwa sababu wale ni watoto na hawana hatia ya kuchukiwa kwa sababu hawana makosa.

download latest music    

katika ukurasa wake wa instagram, Diamond aliandika “……kama vile unipendavyo mimi mama pia uwapende wajukuu zako wote kwani ni wadogo sana na hawana hatia na hawaju chochote ingawa kuna muda wazazi wao wanakukwaza sana kutokana na isssue zetu bibafsi….’

Kwa muda mrefu kumekuwa kukionekana majibizano kati ya bi Sandra na   mama wa watoto waDiamond huku mama huyo akionekana kuwapenda sana watoto wa Zari kuliko yule aliyepo kwa Mobeto.hata hivyo hii sio mara ya kwanza Diamond kuwataka ndugu zake kuwa na upendo na watoto wake kwa sababu yeye tayari ameshakubali kuwa ni wa kwake.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.