Diamond aorodheshwa miongoni mwa wasanii wanaoamini ushirikina

Orodha ya wasanii wanaoamini ushirikina umetolewa, Diamond Platnumz yuko miongoni mwa wasanii waliotajwa kwenye orodha hio.

Meneja Maneno – aliyekuwa meneja wa Diamond, Rich Mavoko, Nay wa Mitego na wasanii wengine, amefunguka kuhusu wasanii anaodai wanaamini ushirikina.

download latest music    

Meneja Maneno anadai kuwa Diamond ndo gwiji wa ushirikina, alikiri kuwa kuna wasanii wengine ambao yeye mwenyewe aliwapeleka kwa waganga wa kienyeji kwa ajili ya kuroga.

Meneja Maneno

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio, Maneno aliwataja pia Rich Mavoko, Sam wa Ukweli miongoni mwa wasanii wanaoamini ushirikina.

“Ndele ni sehemu ambayo baadhi ya wasanii waliiamini sana lakini Mungu akisema ‘Yes’ ni ‘Yes’ tu kwa hiyo nakumbuka wasanii ambao nilikwenda nao kwa waganga kuroga ni pamoja na Rich Mavoko tena tulienda mbali kabisa huko Kigamboni ndani ndani huko tumeenda ndugu yangu, nilisharusha nazi katikati yaani usiku ule unajifanya chizi kama umevurugwa.

“Hata Sam wa Ukweli siwezi kukataa, ni watu ambao imani yao iliwapeleka huko lakini mimi nakumbuka kazi yangu niliyokuwa nafanya sikutaka kwenda kwa waganga…. ila sasa huyu Mondi sasa nimepata taabu naye, mara leo twende kwa mjomba, tunapeleka unga, leo tunapeleka mchele na mganga alivyo mshenzi hajawahi kuagiza samaki, yeye ni jogoo, mbuzi,” Meneja Maneno alisema.

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere