Diamond Asherekea Siku Yake Ya Kuzaliwa Hospitali

Ikiwa jana ni siku yake ya kuzaliwa msanii mkubwa nchini Tanzania  Diamond Platinumz amesherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kutembelea wagonjwa katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar Es Salaam, msanii huyo ambae anajulikana kitaifa na kimataifa ameamua kujumuika pamoja na wagonjwa ikiwa kama moja ya kutoa sadaka na shukrani kwa kutimiza miaka kadhaa.

Imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wasanii kufanya sherehe kubwa zinazotawala vinywaji na vyakula mbalimbali katika kumbi za starehe lakini Diamond aliamua kuwa ni lazima kuwakumbuka watu wenye shida pia, ambapo anaamini hata hao waliopo hospitali pia ni mashabiki zake.

download latest music    

Diamond pia aliamua kutoa vifaa vya hospitali vyenye thamani zaidi ya mil.4 ili kusaidia shughuli za kimatibabu ziendelee katika hospitali hiyo.Hata hivyo Diamond ni mmoja wa watu waliozaliwa katika hopitali ya Amana Ilala jijini Dar Es Salaam miaka kadhaa nyuma , ivyo kitendo cha yeye kutoa misaada hiyo ni kama kurudisha shukrani hospitalini hapo.

Akiongea na mwandishi wa gazeti la Mwananchi msanii Diamond Platinumz alisema kuwa aliamua kuja hospitali na kuleta baadhi ya vifaa maana anajua kuwa hata huku wapo watu wengi wenye shida na wanahitaji misaada pia”najua hospitali kuna mahitaji mengi , nikaona kwa uwezo wangu mdogo  nami nishiriki  kusaidia mahali nilipozaliwa, ili nipate fursa ya  kuwaona pia watoto waliozaliwa siku kama yangu” alisema Diamond

Kwa kipindi kifupi ambacho msanii Diamond alichokuwepo hospitalini hapo, baadhi ya shughuli zilishindwa kuendelea kutokana na hamu ya mashabiki walikuwa hospitalini hapo tukata kuwa karibu na msanii wao.Hata hivyo baada ya shughuli ya kutembela wagonjwa Diamond alipata nafasi ya kufanya sherehe  kwa ajili ya kujumuika na baadhi ya ndugu, jamam na marafiki wa karibu kwa ajili ya kusherekea siku yake hiyo ya kuzaliwa.

Imekuwa ni kama desturi kwa Diamond kutoa misaada au sadaka hizo kwa jamii kimyakimya bila kushirikisha vyombo vya habari, tofauti na baadhi ya wasanii ambao mara nyingi hujikuta wakitaka kutangaza uwepo wao mahali fulani na kusema wanakwenda kufanya nini.Pongezi kwa Diamond na tunamtakia mafanikio zaidi na aendelee na moyo wa kutoa.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.