Diamond Ataja Project Anayoipenda Zaidi Kufanya.

Inawezekana hiki ndicho alichokuwa anataka kukifanya muda wote lakini muda ulikuwa bado haujaruhusu  na  baadhi ya mambo yalikuwa bado hayajakaa sawa kwake,Diamond amekuwa  akisema kila siku  kuwa anapenda sana kusaidia wengine kwa kuwa anaamini kuwa hata yeye amepitia magumu sana mpaka kuwa yeye kama yeye.

Diamond anaamini kuwa wapo vijana  wengi mitaani wamekuwa wakiangaika sana kuendelea na kuvitambulisha vipaji vyao kama ndio njia ya kujipatia  vipato lakini inakuwa kazi kwa sabau wanakosa mtu wa kuwavuta pale walipo.

download latest music    

Katika ukurasa wake w Instagram Diamond aliweka wazi kitu anapenda kufanya ni project yake mpya ambayo inaanza sasa ya kuwa na media yake mwenyewe, kwa kuwa  anaamini kuwa atawafikia vijana wengi sana na kuwainua wengi kutoka pale walipo.

they asked me, what have been my favorire project of all that have done…i said..NEXT ONE!!…wananiuliza ni project ipi ninayoipenda zaidi katika zote nilizowahi kuzifanya ….nawaambia  ni hii inayofuata ..maana naijua haswa  na niliingojea kwa hamu …na itaniwezesha kuwanyanyua na kubadilisha maisha ya vijana wengi mtaani.-Alithibitisha Diamond katika ukurasa wake wa Instagram.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.