Diamond Athibitisha Kuna Kinywaji Kitaingia Udhamini wa Wasafi Festival.

Msanii Diamond Platinumz amethibitisha kuwa uongozi wake tayari umeshaongea na moja ya uongozi wa kinywaji kimoja ambacho kimeamua kutoa udhamini kwa tamasha lao la Wasafi festival linalotarajiwa kuanza wiki ijayo ya tarehe 24 huko Mtwara likizunguka mikao na nchi mbalimbali.

Ikumbukwe kuwa hii imeleta attention kubwa katika mitandao kwa sababu hapo karibuni msanii Alikiba alitoa ahadi ya kutoa udhamini katika tamasha hilo ikiwa kama njia ya kukubali mualiko aliopewa na msanii huyo kuhudhuria tamasha hilo.

download latest music    

katika ukurasa wake wa instagram, Diamond aliandika ” Managementi imeniambia kuwa kuna kinywaji kesho kinaingia on board kuwa mdhamini mkuu, …wasafi festival2018,,,,,naomba tu na mimi nikiambie kuwa naomba kitengeneze stock za kutosha  maana sio tu kunywewa bali hata pia  kuna wengine watataka kukiongea kwa jinsi nitakavyokipa promo ya kutosha.…”

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.