Diamond azua utata kwasababu ya zawadi aliyompa Professor Jay kwenye harusi yake

Professor Jay na mpenzi wake Grace Mkonja walifanya harusi wikendi iliyopita katika kanisa la Katoliki la St. Joseph jijini Dar Es Salaam.

Diamond alijiunga na shamrashamra za harusi ya Professor Jay kwenye ukumbi wa maakuli, staa huyo wa Wasafi aliwatumbuiza wageni kabla ya kumpa Jay zawadi aliyoleta.

download latest music    

Baba Tiffah aliwashangaza wengi kwa kumpa Professor Jay boksi tano za Diamond Karanga na manukato yake ya Chibu perfume kama zawadi.

Diamond akimpea Professor Jay zawadi zake

 

“Nimekuletea hizi boksi unajua uko kwenye ndoa, ndoa nayo inataka uongeze mwili ili watoto watoke wengi,” Diamond aliambia Professor Jay akimpa zawadi zake.

Tazama video hapo chini uone jinsi Diamond alitumbuiza wageni kwa harusi ya Professor Jay:

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere