Diamond karanga yaanza kuuzwa Kenya pia

Diamond Platnumz alizindua bidhaa yake mpya ‘Diamond Karanga’ baada ya kumlaki sta wa Wasafi – Rayvanny kutoka Marekani.

Kuzinduliwa kwa Diamond Karanga uliwashangaza watu wengi kwani Baba Tiffah alianza tu kuuza manukato yake ‘Chibu Perfume’ miezi michache iliyopita.

download latest music    

Diamond sasa anauza karanga zake Tanzania nzima na ata Kenya pia; staa huyo amesema Diamond Karanga zauzwa Mombasa kwa sasa.

“USISEME KARANGA SEMA DIAMOND KARANGA!!!!…Habari njema kwa Vijana wenzangu wote, sasa unaweza kujipatia Mtonyo wa ChapChap kupitia @diamondkaranga ambapo utaweza kununua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu ishirini (20,000) kwa boksi moja lenye pakiti Mia moja (100) ndani ambazo ukiuza unapata faida ya elfu kumi fanya mawasiliano sasa na mawakala walio karibu yako. Mawasiliano kwa Kununua Jumla:- MOMBASA +254700187727” aliandika Diamond.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere