Diamond Na Rick Ross Kufanya Ngoma Ya Pamoja

Msanii mkubwa kutoka Tanzania Diamond Platinumz anatarajia kufanya kazi pamoja na msanii mkubwa duniani na anaejulikana kama msanii mkubwa na tajiri Duniani  Rick Ross.Kwa muda sasa wasanii hao wamekuwa wakionekana kuwa na mahusiano ya karibu kwa sababu ya wote kuwa mabalozi wa kinywaji cha Belaire ambacho kinatengeneza nchi za Ulaya.Rick Ross amekuwa akimpost Diamond katika kurasa zake za mitandao ya kijamii zaidi ya mara moja huku akimpongeza kwa sikukuuu ya kuzaliwa na kumkaribisha katika ubalozi wa kutangaza kinywaji hicho.

Akiandika na kupost kipande cha video kinachoonyesha wasanii hao wapo pamoja wakiimba  katika ukurasa wake wa Instagram, meneja wa Diamond Platinumz, Sallam K alirusha video iyo na kuthibitisha kuwa wawili hao  wapo katika maandalizi  na wanatarajia kutoa  kazi yao  wakiwa pamoja.Kipande hicho kinaonyesha wapo  katika moja ya location .

download latest music    

Sallam K aliandika “Diamond Platinumz x Rick Ross on set now  somewhere in Miami  #BlackBottleBoys and we never stop!!!” alituma meneja wa diamond,

Diamond Platinumz kutoka Tanzania  akiwa katika picha ya pamoja na Rick Ross wa Marekani  na msanii mwenzie kutoka Tanzania Rayvanny.

Diamond ambae kwa sasa yuko nje ya nchi alikoenda katika tuzio za AFRIMA na kushindwa tuzo mbili katika vinyanganyio tofauti amekuwa ni mmoja wa wasanii wakubwa bongo wanaofungua mipaka na kufanya kazi na wasanii wakubwa kutoka nje,hivi karibuni Diamond Platinumz alitoa wimbo mpya unajulikana kwa jina la Hallellujah aliowashirikisha kundi kubwa la muziki  Duniani linalojulikana kama Morgan Heritage na wimbo huo umekuwa ukifanya vizuri katika vituo vya  radio na televisheni.

Akiwa balozi mkubwa wa muziki kutoka nchini Tanzania Diamond amekuwa akijitaidi kufanya vizuri katika muziki na kusaidia hata wengine wanaotaka kuendelea katika muziki kwa kuanzisha lebel yake ya Wcb inayoibua wasanii wakubwa na  kujulikana Afrika na duaniani kwa ujumla.Diamond amekuwa ni msanii anaeweza kuthubutu kufanya kitu chochote ili kukuza muziki wake na Tanzania kwa ujumla.Yeye ni msanii wa kuigwa na wasanii wengine

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.