Diamond Platnumz aeleza kwanini amechelewesha uzinduzi wa headphones zake

2017 ilivyoanza Diamond alisema atazindua bidhaa kadhaa na alianza na manukato ‘Chibu Perfume’ kisha hivi karibuni alianza kuuza karanga – ‘Diamond Karanga’.

Staa huyo wa Wasafi sasa anafuata nyayo ya wasanii wa kimataifa kama Dr. Dre na 50 Cent walioingia kwenye biashara ya headphones.

download latest music    

Diamond alitangaza ujio wa ‘Chibu Beats’ lakini hakuweza kuzindua headphones hizo kwa sababu ya umiliki wa jina ‘beats’.

“Katika usajili wa Chibu Beats jina lilileta matatizo kidogo, ilikwamisha hapo kwa sababu neno beats mtu kashalisajili dunia nzima mtu mwingine asilitumie neno la beats, siunajua ni la Dre. Kwa hiyo tunaweka namna nyingine ambayo itakuwa nzuri, zitatoka zimeshakuwa tayari mpaka sampo, tumeshasikiliza ni fresh sound hatari” amesema Diamond akiwa katika kipindi ya XXL ya Clouds FM.

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere