Diamond Platnumz aeleza kwanini vijana wanashindwa kuingia Wasafi Records

Ni wengi ambao wanatamani kujiunga na label ya Wasafi Records. Hata hivyo kulingana na sheria ambazo Diamond Platnumz ameziweka wasanii wachache ndio tu wamehitimu

Akizungumza kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm Diamond Platnumz alisema kuwa yeye hutaka wasanii ambao wanaubunifu wa kujiandikia nyimbo kwa sababu hii inasaidia kuangalia maudhui na uzuri wa wimbo.

download latest music    

“Kwanza Rich Mavoko ndiye mgumu kwenye kupitisha nyimbo, ikitoka hapo Ravvanny aipitishe, Queen Darleen aipitishe, ikitoka hapo niipitishe mimi, iende kwa Mkubwa Fella na Babu Tale waipitishe na Sallam aipitishe, ukitoka hapo wewe ni mwanaume haswa.”

Diamond aliendelea kwa kusema,

“Kwa hiyo wengi wanakuwa na uwezo mkubwa. Labda unaweza ukaja ukasikia kitu kidogo, ukasema ukiweka hapa kitu flani itakuwa poa zaidi, yaani ukiandika unaandika haswa.”

Lakini kwa sasa Diamond Platnumz amemsign Lava Lava ambaye amenonekana kuwa mkali baada ya kuachia wimbo wake mpya.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua