Diamond Platnumz aeleza sababu hataki Tiffah awemsanii kama yeye

Wasanii wengi duniani hawapendi kuwaonyesha Watoto wao mitandaoni na ukiwaukiza, hii ni kwa sababu wanahofia watoto wao kuishi maisha kama wanayoishi.

Mmoja wao ni Diamond Platnumz ambaye anahofia mwanawe, Tiffah Dangote kuwa msanii. Akizungumza kwenye mahojiano na Larry Madowo wa NTV Kenya Diamond alisema kuwa Tiffah akiwa msanii atatembea na wanaume wengi kitu ambacho yeye mwenyewe hataki kukiona ama kusikia. Alisema,

download latest music    

“Mtoto wangu wa kiume ningependa awe msanii lakini mtoto wangu wa kike sitaki awe msanii, watamla sana. Mtoto akiwa msanii watu wanaomjua wanakuwa wengi, watu wanaokujua wakiwa wengi na kutongozwa kunakuwa kwingi, sasa watanipa presha. Ukiwa mwanaume lijali na ukiwa kwenye nafasi kama yangu lazima wataliwa. Nilikuwa kwenye kutafuta tafuta, mpaka nilivyompata Zari na kweli nimetulia,”

Tazama interview hiyo hapa:

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua