Diamond Platnumz aendelea kuwakanganya wengi kwa kingereza chake

Image: Diamond Platnumz

Sio kila mtu ambaye alibarikiwa kujua kingereza akiwa mdogo na ndio maana kuna watu ambao bado hata sasa hivi bado wanapata shida kuwasilia na wenzao kwa kutumia lugha hii.

Mmoja wa hawa ni Diamond Platnumz ambaye amekuwa mitandaoni kwa kuwachanganya mashabiki wake anapoandika ujumbe wa kingereza kupitia mtandao wake wa Instagram.

download latest music    

Msanii huyu amerudia kosa hili baada ya kuweka picha ya manukato yake na kuandika ujumbe ambao haueleweki kwa kutumia lugha ya kingereza. Aliandika kusema,

i wish you know, how in Love i am with this fragrance …. CHIBU PERFUME!!!! by @diamondplatnumz #TheScentYouDeserve Artwork and ? by @kifesi @chibuperfume

Hata hivyo mashabiki wake hawakumpa nafasi ya kupumua walipoanza kumponda na kumcheka mkali huyu wa wasafi. Mmoja aliandika Broo wengine hatuja soma hatuelewi kizungu jaribu kutuwekea na lugha yetu ya kiswahili tunafuatilia Sana habari zako tunahitaji kujua.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua