Diamond Platnumz Amepata Skendo Nyingine Safari Hii na Mrembo Tunda

Model na muuza nyago kwenye video maarufu Kama Tunda the bossbabe amejikuta katika skendo na Msanii maarufu wa kizazi kipya Diamond Platnumz baada ya habari kuenea kuwa amebeba ujauzito wa Diamond.

Waswahili wanasema lisemwalo lipo na kama halipo basi laja. Msemo huu umedhihirika tena kwa msanii pendwa na supastaa anayependwa kuongelewa sana bongo na si mara zote anaongelewa kwaajili ya mziki wake bali mara nyingi ana-make headline kwa maisha yake binafsi ya kimahusiano.

download latest music    

Diamond amerudi tena kwenye skendo na mrembo mwingine anayejulikana kama Tunda anayedaiwa kuwa na uhusiano naye wa kimapenzi na kinachowavutia wengi ni kuwa inasemekana kuwa Tunda ana ujauzito wa Diamond.

Habari hizi zimeenea kwa kasi ya ajabu kwani Tunda amekuwa akiweka picha za Diamond kwenye ukurasa wake wa Instagram kila kukicha kitendo kinachowafanya watu waamini kuwa Tunda ana uhusiano wa kimapenzi na Diamond.

Baadhi ya picha za Diamond alizoweka Tunda kwenye ukurasa wake wa Instagram ni hizi:

Siku za nyuma tetesi ziliwahi kuenea kuwa Diamond ana uhusiano na Tunda kitendo ambacho kilikanwa mara moja na mti wa karibu Wa Diamond na kudai kuwa ni jitihada za wait kusambaza maneno ya uongo ili waweze kumgombanisha Diamond na mama watoto wake na kipenzi chake Zari, lakini hivi sasa inasemekana kuwa sio tu tetesi kwani baada ya miezi tisa mnaweza mkamuona Diamond akielekea tena kwenye vyombo vya habari kumkubali mtoto.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.