Diamond Platnumz amuandikia Ray C ujumbe kumpa moyo wa kutokata tamaa katika muziki wake

Image: Diamond Platnumz

Ni wengi ambao hawakudhania kuwa Ray C atarudi kufanya muziki tena baada ya kupotea ndani ya madawa ya kulevya. Hata hivyo mrembo huyu amewafurahisha wengi ambao hawakuwa wamekata tamaa kwake.

Mmoja wa hawa ni Diamond Platnumz ambaye amemwandikia ujumbe wa kumtia moyo huku akimsihi kuendelea na muziki wake japo ya kukawia sana bila kutoa nyimbo.

download latest music    

Kupitia mtandao wa Instagram Diamond aliandika kusema…

Ray C

Salaam dada angu @rayctanzania , siku ya leo nilitamani nikwambie maneno haya: Spirit ama juhudi unayoionyesha sasa inatia faraja sana, naamini sio kwa wapenda muziki wa Tanzania tu bali hata kwa watu mbalimbali…. Nafarijika kuona wimbo wako wa #Unanimaliza watu mbalimbali wameupokea vizuri, na nisiwe mnafiki hata mie ni miongoni mwa watu wanaoupenda wimbo huu wako mpya….

Diamond aliendelea kwa kusema,

Ombi langu kwako usikubali kurudi nyuma tena, ijapokuwa sanaa zetu zina changamoto nyingi ila amini ni mitihani tu ya Mwenyez Mungu, ila ukiwa mvumilivu na kumuomba Muumba, itapita….niwaombe pia Vyombo vya Habari vyetu pendwa tuzidi kumsapoti dada etu, kwani naami kwa sapoti yenu, sapoti ya wadau mbalimbali na kuongeza juhudi kwake kutamfanya awe mfano bora, na kuamsha vijana wengi sana mitaani kwetu ambao pengine walijikatia tamaa kwa mambo mbalimbali….InshaAllah Mwenyez Mungu akusmamaie katika kazi zako na Maisha ya kila siku? @rayctanzania

Hata hivyo Ray C ameonyesha kuwa hanamipango ya kuacha muziki tena na kuna uwezekano wa kuenda mbali hivi karibuni.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua