Diamond Platnumz: Nampenda Zari na Siwezi Kumuacha

Mwanamuziki machachari wa Bongo fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ amefunguka na kudai kuwa anampenda sana mpenzi wake Zari na hawezi kumuacha.

Wiki iliyopita ilikuwa ni wiki ya Diamond kwani alikuwa akitawala vichwa vya habari vyote kwenye mitandao ya kijamii sababu ya uhusiano wake na mama watoto wake Zari.

download latest music    

Baada ya habari kusambaa kuwa Diamond ana uhusiano wa kimapenzi na mrembo anayeitwa Tunda kuna tetesi zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kuwa Diamond na mpenzi wake Zari wameachana.

Siku chache zilizopita Diamond alitua nchini Rwanda ambako ameenda kwa ajili ya kutambulisha bidhaa zake za Chibu perfume na Diamond karanga, bidhaa ambazo tayari ni maarufu sana nchini Tanzania, Kenya na Uganda.

Kwenye mkutano na waandishi wa habari (press conference) nchini Rwanda, Diamond alifunguka kuhusu suala linalozungumzwa sana mtandaoni nalo ni uhusiano wake na Zari kwa hivi sasa ambapo Amesisitiza kuwa ana mwanamke mmoja tu ambaye ni Zari na anampenda sana na hategemei kumuacha.

Lakini pia Diamond amefunguka na kutaja idadi ya watoto aliokuwa nao na amesema kuwa ana watoto watatu ambao ni Tiffah na Nillan aliozaa na Zari na Dylan aliyezaa na Hamisa. Hii imetokana na wanawake wengi kujitokeza na kudai kuwa wamezaa na Diamond.

Diamond alimalizia kwa kuongelea album yake mpya inayoitwa ‘A boy from Tandale’  ambayo anategemea kuitoa tarehe 23  mwezi wa pili ambapo kwenye albamu hiyo amewashirikisha wasanii wakubwa kama Rick Ross.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.