Diamond: Wasafi hairuhusu wasanii wake kuandikiwa nyimbo

Wasanii wengi maarufu duniani huandikiwa nyimbo zao, kwa mfano Ne-Yo ingawaje ni mwimbaji ambaye ametajika, anajulikana pia kuandikia wasanii wenzake nyimbo.

Ne-Yo aliandika ‘Take a Bow’ iliyoimbwa na Rihanna, ‘Spotlight’ ya Jennifer Hudson, ‘Irreplaceable’ ya Beyonce, ‘Knock You Down’ ya Keri Hilson na nyimbo zingine kadhaa.

download latest music    

Hata kama imedhibitishwa kuwa wasanii wanaweza fanikiwa kimuziki bila kuandika nyimbo zao, Diamond hataki msanii kujiunga na lebo yake kama hajui kuandika nyimbo.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds Fm, Diamond alisema wasanii kutoka Wasafi huandika nyimbo zao wenyewe. Aliongezea kusema kwamba kabla ya kurecord wimbo wowote, wasani wote wa Wasafi hukagua wimbo aliyoandika msanii ili kubaini kama kuna makosa na kuelekezana.

“Kwanza Rich Mavoko ndiye mgumu kwenye kupitisha nyimbo, ikitoka hapo Ravvanny aipitishe, Queen Darleen aipitishe, ikitoka hapo niipitishe mimi, iende kwa Mkubwa Fella na Babu Tale waipitishe na Sallam aipitishe, ukitoka hapo wewe ni mwanaume haswa. Kwa hiyo wengi wanakuwa na uwezo mkubwa. Labda unaweza ukaja ukasikia kitu kidogo, ukasema ukiweka hapa kitu flani itakuwa poa zaidi, yaani ukiandika unaandika haswa,” ameeleza Diamond.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere