Diamond: Watu hawajui mimi na Wema Sepetu tunaongea sana lakini sio kwenye media

Diamond and Wema Sepetu walikua wapenzi kabla ya hit maker huyo kumtema Wema na kumoa Zari Hassan, hatua ambayo ilizua utata sana.

Watu wengi waliamini kuwa Diamond alitaka mtoto ndo maana alimwacha Wema Sepetu ambaye mbaka wa leo hajajaliwa kupata mtoto.

download latest music    

Hata kama Diamond alimwacha Wema, wawili hao bado huwa wanaongea na kukutana bila ya vyombo vya habari kupata uhondo wowote.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond alidhibitisha kuwa bado ako na uhusiano mwema na Wema Sepetu ingawa wao hufanya vitu vyao jini ya maji.

Hit maker huyo wa ‘Marry You’ alifunguka na kusema kuwa yale maneno ya kuvutia kwenye manukato yake – ‘The scent you deserve’ ni Wema Sepetu ndo alitoa.

Chibu Perfume

“Mimi na Wema labda watu hawajui sisi tunaongea sana wakati mwingine tunakutana tu sana lakini sio kwenye media. Tushakuwa kila mtu ana mahusiano yake tofauti yeye ana familia yake hata ukiangalia katika Perfume yangu lile neno THE SCENT YOU DESERVE alilitoa Wema” alisema Diamond.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere