Dida: Sitaki Hata Kusikia Masuala Ya Ndoa

Mtangazaji mkongwe wa kipindi cha Taarabu, Times Fm Khadijah Shabibu maarufu kama Dida amefunguka na kuweka wazi kuwa hana mpango wa kufunga ndoa.

Dida ambaye ameshafunga ndoa tatu na kuachika amesema kuwa hataki kusikia kitu kinachoitwa ndoa kwani anaona kama inamuongezea maradhi ya vidonda vya tumbo hivyo ni bora ajikite kwenye kutafuta fedha.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers , Dida alisema ameamua kuachana na habari za ndoa licha ya kwamba alivishwa pete ya uchumba lakini aliamua kumwagana na jamaa wake huyo akidai dunia ya sasa siyo ya kuolewa tena.

Kwa sasa ukiniambia habari za ndoa kwa kweli sikuelewi kabisa maana sitaki vidonda vya tumbo na presha, akili yangu inawaza kutafuta fedha na jinsi ya kumsomesha mwanangu afike mbali aje anitunze mambo mengine nimetupa kule”.

Baada ya kuwa kwenye ndoa mara tatu na zote kuvunjika Dida alibahatika kuvishwa tena pete ya uchumba mwaka jana na Mwenyekiti wa Kijiji cha Ukuni, Bagamoyo, Issa Seleman lakini uchumba huo ulipotea.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.