Diva Adhamiria Kushika Ujauzito Mwaka Huu Kwa Njia Yoyote

Mtangazaji machachari wa kipindi cha Ala za roho kinachoruka Clouds Fm Loveness Malinzi maarufu kama Diva the Bawse ameibuka na kuwaambia mashabiki zake kuwa amedhamiria kushika mimba mwaka huu kwa njia yoyote ile.

Diva amekuwa kwenye headlines sana kwenye mitandao ya kijamii tangu mwaka umeanza hii ilitokea baada ya yeye na mpenzi wake wa zamani Heri Muziki kukorofishana ndani ya studio za Clouds Fm kwenye kipindi cha Leo Tena.

download latest music    

Wawili hao walienda studio hapo kwa ajili ya mahojiano kuhusu mziki wa Heri Muziki na mapenzi yao kwa ujumla lakini walipofika studio mule Heri hakutaka kuongelea mapenzi yake na Diva bali alitaka kuongelea mziki na kuishia kusema  yeye na Diva hawana mahusiano.

Bifu lile lilikuwa kubwa na Diva alionekana ku-mind sana kwani baada ya ugomvi huo wawili hao walitangaza kuachana na Heri Muziki alikuwa wa kwanza kusema kuwa yeye ndiye aliyemuacha Diva.

Diva ni moja kati ya mastaa ambao wanapenda sana kuweka mambo yao hadharani hasa kwenye mitandao ya  kijamii huku hilo likiwa ni jambo la kawaida sana kwake sasa jana amewaacha hoi mashabiki zake kwenye mtandao wa Twitter baada ya kutangaza anahitaji kushika mimba mwaka huu kwa njia yoyote na kuwataka mashabiki zake waanze kuhesabu siku:

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Diva aliandika maneno haya:

Tangazo mwaka huu lazima niwe na ujauzito By any means…. Anzeni count down”.

Baada ya kutoa tangazo hili la kushika ujauzito mashabiki zake wengi walionekana kushangazwa na yeye kuwataka waanze kumuhesabia siku za kushika mimba.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.