Diva Nae Aibuka na Jina la Tanzania SweetHeart

Kwa muda mref warembo Wema Sepetu na Hamisa mobeto wamekuwa wakigombania jina la kuwa Tanzania Sweetheart jina ambalo alipewa Wema miaka ya nyuma na mashabiki zake kutokana na kupendwa sana na mashabiki zake na tanzania nzima kwa ujumla, hata hivyo jina hilo kwa sasa linaonekana kulegalega baada ya mashabiki wa Hamisa pia kutoka kumkabidhi jina hilo msanii wao hamisa.

Vita hii ya jina imekuwepo kwa muda mrefu mpaka kufikia hatua ya baadhi ya mastaa kuingilia kati na kila mmoja kusema msimamo wake huku wengi wakitaka libaki kwa mwenyewe Wema , hata hivyo baadhi ya watu hao ni pamoja Diva the bawse ambae ameibuka lakini kwa kutaka kumtetea Hamisa.

download latest music    

Tanzania sweetheart, africa sweetheart, word sweetheart, asietaka anywe panadol extra,  ndo nishasema point blank period, mi sipendi kabisa tabia ya kupindisha  maneno nimeyaweka wazi kabisa kuwa my baby @hamisa mobeto  came through dripping, we nyoosha tu baby,..hakuna namna we damshi tu kote , am so proud of hard working mama….jamani you all know kuwa mimi sina matatizo na mtu maana mapovu kama yote.

Diva anasema kuwa watu watamshangaa kuona akimtete Hamisa lakini wakae wakijua kuwa yeye na hamisa ni marafiki wa muda mrefu sana na kwamba ushoga wao umekuwa prvate kila siku kwa sababu sio lazima kila mtu ajue.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.