Dk Fadhili Emily: Kama singekua nimeokoka ningemuoa Jacqueline Wolper

Mpenzi wa zamani wa Jacqueline Wolper amefunguka na kusema kuwa mrembo huyo anafaa kuwa mke wa mtu. Dk Fadhili Emily amemsifu Wolper kwa kusema kuwa muigizaji huyo anaweza akawa mke mwema kwa atakaye muoa.

Fadhili alisema haya baada ya kuzuka kwa madai kuwa Wolper hawezi kuolewa kwasababu ya yeye kuwa na msururu wa wanaume ambao amekua na mahusiano nao. Fadhili alieleza kuwa angemuoa Wolper lakini yeye sasa ameokoka na pia amepata mpenzi mwingine.

download latest music    
Dk Fadhili Emily na Wolper kwenye picha ya zamani

“Nimeona kwenye mitandao, wanamuandama kuwa hajatulia na kwamba ana msururu mkubwa wa wanaume ambao ametembea nao, kimsingi huyu mrembo hajapata tu mtu sahihi lakini anafaa kuwa mke wa kulea familia kabisa,” alisema Fadhili.

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere