Dogo Janja amkana Muna Love baada ya tetesi kuwa wawili hao ni wapenzi

Dogo Janja amefunguka kuhusu uhusiano wake na muigizaji wa filamu Muna Love. Akizungumza kwenye interview hivi karibuni Dogo Janja alisema kuwa yeye na mrembo huyo hawana uhusiano wowote wa kimapenzi Kama wengi wanavyodhania.

Muna Love

Msanii huyo wa Bongo alidai kuwa tetesi hizi ni za uongo. Aliendelea kwa kusema kuwa uvumi huu umemuumiza na pia familia yake. Dogo alisema,

download latest music    

“Hakuna kitu kibaya kama utandawazi, yaani kila mtu ana simu na bando lake kwa hiyo akiamka asubuhi anajisikia kufanya chochote au kutunga vitu kama hivyo lakini siyo kitu kizuri, maana yananiumiza mimi na familia yangu, Uongozi wangu lakini pia vinamuumiza mpenzi wangu kwa sababu tuna malengo makubwa hivyo haya yanapoendelea yanazidi kumuumiza au kumchanganya”,

Aliendelea kwamba,

“Mimi siyo mtu wa kuonesha maisha yangu binafsi kwenye mitandao ndio maana hata mpenzi wangu sijawahi kumuweka mitandaoni, maisha yangu binafsi ni ya kwangu na siyo ya kila mtu hata huyo dada wa watu anaumizwa na hili na anafamilia pia kwa hioyo hizi habari zinazidi kumuweka pabaya.

About this writer:

Pauline Syombua

Content Developer IG: Kermbua