Dogo Janja: Davido ako na pesa lakini hajui kuvaa

Rapper Dogo Janja amemshambulia Davido kwa kile alichodai kuwa msanii huyo kutoka Nigeria hajui kuvaa licha ya kuwa na utajiri mkubwa.

Dogo Janja ni miongoni mwa wasanii wanaong’ara sana nchini Tanzania, hivi karibuni alipigiwa upata kuwa anang’ara sana kushinda Diamond Platnumz.

download latest music    
Davido

Soma pia: Picha 10 za Dogo Janja ambazo ni dhibitisho kuwa anang’ara kimavazi kushinda Diamond Platnumz

Akiongea akiwa Sibuka FM, Dogo Janja alisema Davido ako na pesa nyingi lakini hajui kupendeza kimavazi, alieleza kuwa mara nyingi nguo anazovaa Davido ni kama huwa zimetundikwa tu mwilini mwake.

Janja pia alisisitiza kuwa yeye ndiye anayeng’ara zaidi kushinda wasanii wote nchini Tanzania. Aliwataja G Nako, Jux kwa mbali na Joh Makini kama wapinzani wake kwa uvaaji.

Dogo Janja

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere