Dogo Janja na Uwoya Wahama Nyumba Kisa Mzimu wa Masogange

Msanii wa Bongo fleva Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja na mkewe staa wa Bongo movie Irene Uwoya wamehama nyumba waliyokuwa wanaishi ili kukimbia mzimu wa Agnes Masogange.

Agnes Gerald au maarufu kama Masogange aliaga dunia Miezi miwili iliyopita kutokana na maradhi ya pumu.

download latest music    

Rafiki mkubwa wa Masogange alikuwa Uwoya ambaye pia walikuwa wanaishi pamoja maeneo ya Makongo Juu.

Lakini sasa Wanandoa hao wanafunguka kuwa sababu iliyowapelekea mpaka kuhama nyumba yao ya zamani ni kukimbia mzimu wa Masogange ambao walikuwa wanahisi kuuona.

Kwenye mahojiano na Clouds Tv, Dogo Janja  amesema wamelazimika kuhama nyumba hiyo na kwenda kupanga nyumba nyingine ambayo hulipa US Dollar 800 kwa mwezi kutokana na umbali, pili mkewe, Irene alikuwa akisumbuliwa na kumbumbuka za mara kwa mara kuhusu marehemu Agnes Gerald ‘Masogange’.

Nahisi kama nilikuwa namuona hivi, kwa hiyo nikashindwa, eeeh!! mara nyingi pia nahisi kama anapita hivi“.

Dogo Janja na Uwoya walianika nyumba yao kifahari kwa wageni wao walioalikwa kufuturu wikiend iliyopita.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.