Dogo Janja: Tupo Bize Tunakesha Tukitafuta Mtoto

Mwanamuziki wa Bongo fleva anayefanya vizuri na ngoma yake ya wayuwayu Dogo Janja amefunguka na kuweka wazi kuwa yeye na mke wake staa wa Bongo movie Irene Uwoya wanatafuta mtoto.

Uwoya ambaye tayari ana mtoto mmoja Krish aliyezaa na marehemu Ndikumana Kataut amedai yuko katika jitihada za kumtafutia Krish mdogo wake.

download latest music    

Kwenye mahojiano  na Ijumaa Wikienda, kwa nyakati tofauti mastaa  hao walifunguka kuwa, kwa kipindi hiki cha mvua ndiyo muda sahihi wa kusaka mtoto hivyo wanalifanyia kazi suala hilo kwa nguvu zao zote.

Tupo bize kidogo, tunasaka mtoto maana si unajua watu wanaangalia matunda ya ndoa kwa jicho la tatu hivyo sisi tunaangaika na hilo sasa hivi,” alisema Dogo Janja

Lakini pia Uwoya naye alifunguka na kusema ni haki yake kumpatia mtoto mume wake kama wanandoa lakini hasa hivi sasa anahitaji kumpa mdogo wake Krish kwani ameshakuwa mkubwa.

Mke lazima amzalie mumewe na mimi na mume wangu sioni tunachosubiri kwa sasa maana Krish ni mkaka mkubwa na anahitaji mdogo wake“.

Irene Uwoya na Dogo janja walifunga ndoa mwaka jana mwishoni.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.