Dude Amwaga Povu Kwa Mashabiki Zake

Muigizaji wa Bongo movie Kulwa Kikumba maarufu kama Dude ameshindwa uvumilivu na kuamua kuwajibu mashabiki ambao wamekuwa wakimponda kwa Kitendo Cha kuposti picha akiwa anaswali.

SIku chache zilizopita Dude aliweka picha Kwenye ukurasa wake wa Instagram Ikiwa inamuonyesha akiwa anaswali jambo ambalo liliwakera mashabiki zake wengi.

download latest music    

Mashabiki walimjia juu Dude wakidai Dini hairuhusu mtu kujipiga picha ukiwa unafanya Ibadan halafu uje uweke Kwenye mitandao ya kijamii kwa nia ya kujionyesha.

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Dude amewajibu mashabiki kuwa alifanya hivyo ili kuwashawishi wengine kumcha Mungu.

Watu huwaona wasanii kama siyo wacha Mungu, kupiga picha nikifanya ibada kinawa­kumbusha wafuasi wangu wenye imani kama yangu ya Kiis­lamu kumkumbuka Allah”.

Dude sio msanii wa kwanza kukosolewa baada ya kuposti picha mitandaoni akiwa anasali kwani siku za nyuma Wastara alipata kichambo kama hiko baada ya kiposti picha akiwa anaswali.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.