Dudubaya Akiri Kumkubali Gigy Money

Msanii mkongwe wa Muziki wa Bongo fleva Tumaini Godfrey maarufu kama Dudubaya ameibuka na kuweka kuwa anamkubali msanii mwenzake Gigy Money.

Dudu Baya amesema kuwa msichana anayeweza kumuoa na anampenda ni Gigy Money na Lady Jaydee. Japo kuwa ameeleza kuwa Gigy anatabia ambazo bado haweki kumfanya awe mke labda aziache.

download latest music    

Mwanamke ninayempenda ni Gigy Money, Gigy huwa nampenda ila tabia zake ambapo bado siwezi kumfanya kuwa mke yaani mpaka aache zile tabia, tulishazungumza ila hawezi kuacha zile tabia, Gigy mnaweza mkawa sehemu akaanza kucheza akiwa uchi kwahiyo kama mama watoto siwezi.

Lakini tukija mabinti wengine wakike kwenye hustle anajiamini ni Lady Jaydee, kwasababu ni mwanamke mwenye akili timamu kwasababu mimi nampenda mwanamke mbishi kwasababu mimi ni Konki”.

Dudubaya na Gigy Money waliwahi kuibua Tetesi Za kuwa pamoja Baada ya kuonekana karibu kuliko kawaida walipokuwa pamoja kwenye ziara ya Wasafi Festival.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.