Dudubaya Atoa Tamko Kwa Vyombo Vya Habari Kuhusu Mwanaye Wille

Msanii mkongwe wa Bongo fleva Dudubaya aliyewahi kutamba na vibao vyake kama Mpenzi na Nakupenda amemwaga povu zito kwa vyombo vya habari kuhusu Mahusiano Yake na mwanaye Wille.

Kwa muda mrefu sasa Dudubaya amekuwa hana uhusiano mzuri na mtoto wake Wille ambapo imedaiwa kuwa aliamua kumtelekeza mtoto huyo kwa kama yake baaada ya kuacha shule na kuamua kufanya Muziki.

download latest music    

Lakini sasa baada ya mgogoro wa muda mrefu na mvutano Kwenye mitandao ya kijamii Dudubaya ameweka wazi kuwa hataki tena kuulizwa na vyombo vya habari kuhusu mtoto wao wake.

Kwenye mahojiano na Kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Dudubaya ametangaza rai hii:

Leo tarehe 18 mwezi wa 6 mwaka 2018 natangaza kauli yangu kwenye vyombo vya habari kuwa sitaki Dj yoyote, mtangazaji yoyote aniulize kuhusu mtoto wangu Wille kwa sababu toka ameacha shule hayuko mikononi mwangu yuko kwa mama yake na kila kitu atakachofanya huko mimi sitahusika”.

Siku za hivi karibuni kuna picha zilisambaa Kwenye vyombo vya habari zilizomuonyesha Wille akiwa anavuta bhangi na kunywa pombe.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.