Dudubaya na Gigy Money Wabambwa Pabaya

Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudubaya amedaiwa kukutwa chobingo na msanii mwenzake Gigy Money wakiwa wanafanya yao.

Global Publishers wanaripoti kuwa pamoja na ugumu wote ambao Dudubaya anadaiwa kuwa nao lakini alikutwa akiwa anachekeshwa na kukalishwa na Mtoto Gigy.

download latest music    

Wawili hao walinaswa nyuma ya jukwaa la Wasafi Festival katika tamasha lililofanyika Uwanja wa Nelson Mandela uliopo Halmashauri ya Mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa mbapo Gigy alikuwa ameshapanda jukwaani na kuwapa burudani wakazi wa eneo hilo. Katika tukio hilo, wawili hao walinaswa wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba huku kila mmoja akionekana kukolea kwa mwenzake.

Baada ya kuzua gumzo mbele za watu ndipo waandishi wa Gazeti la Risasi Mchanganyiko liliwafuata wawili hao lakini waliomba waachwe wapumzike kwa madai kwamba walikuwa wamechoka kuhojiwa.

Hebu tuache bwana tupumzike…”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.