Duma Akiri Kumkubali Sana Johari

Msanii wa filamu za kibongo Daudi Michael maarufu kama Duma amefunguka na kukiri kuwa hakuna msanii wa kike anayemkubali kama anavyomkubali Johari.

Duma amekiri kuwa Msanii huyo mkongwe (Johari) ndio aliyempa yeye hamasa ya kuweza kuingia kwenye filamu miaka ya nyuma.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Duma amesema kuwa hata akiulizwa mahali popote kuhusu msanii aliyemfanya aingie kwenye uigizaji hawezi kuona aibu kusema ni Johari kwa sababu mpaka leo hii ndio msanii wa kike anayempenda sana.

Siwezi kuwa mnafiki hata kidogo ukweli ni kwamba Johari ndiye aliyenifanya niingie kwenye tasnia ya filamu kwa sababu alikuwa akiigiza kiuhalisia kwenye filamu yake ya Johari na mpaka leo ni mwanamke wa kwanza kumpenda Bongo Muvi“.

Johari alijizolea umaarufu miaka ya nyuma Kupitia maigizo kadhaa aliyokuwa anafanya na ambapo alikuwa anaigiza na wasanii kama Ray, Marehemu Kanumba na wengineo.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.