Duma-Bongo Movie Inakuwa na Wasanii Tunafaidika

Msanii wa filamu za Bongo Movie Daud Michael maarufu kwa Jina la usanii kama Duma amefunguka na kudai sanaa ya Bongo Movie inakuwa kwa kasi.

Duma ambaye alifanya uzinduzi wa filamu yake mpya ya Nipe Changu amedai kwa sasa Kikula kwa filamu za kibongo ni kwa kasi kubwa Lakini pia wasanii wanaona faida.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Global Publishers, Duma Duma alisema sanaa ya Tanzania kwa sasa inakua na anaona jinsi ambavyo wasanii watanufaika.

Niseme tu kwamba nashukuru kwa sababu mifumo inayokuja ni ya faida, siyo mifumo ya kuuziana haki miliki hivyo naamini kila msanii ambaye atafanya kazi zake vizuri, anakwenda kunufaika nazo, kikubwa ni kumuomba Mungu ili tuweze kufikia malengo”.

Kauli hii ya Duma inatia moyo kwani kwa muda mrefu sasa tangu Steven Kanumba afariki dunia kumekuwa na pengo kubwa katika sanaa hiyo na hata watu kudai Kanumba alikufa na Matumaini ya kukua kwa sanaa.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.