Ebitoke Aibua Mapya Kuhusu Penzi lake na Ben Pol

Mchekeshaji kutoka timamu TV Ebitoke ameibuka upyaa na habari za kinachoendelea baina yake na mpenzi wake supastaa wa Bongo.fleva, Ben Pol.

Ben Pol na Ebitoke wamesemekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa muda mrefu lakini mara imeonekana kwamba kuna utata Fulani kwemye mapenzi yao.

download latest music    

Ebitoke alianzisha mahusiano na Ben Pol baada ya kutangaza kupitia mitandao ya kijamii kuwa anavutiwa naye na angependa kuwa na mahusiano naye, baada ya muda mfupi mapicha picha talianza kusambaa mtandaobi zikiwaonyesha wawili hao wakiwa kwenye mahaba mazito.

Miezi michache iliyopita wakati wa tamasha la Fiesta Ebitoke alitangaza kuwa ameamua kuachana na Ben pol kwa sababu ameona kama ni mtu ambaye haeleweki au hataki kuwa na yeye kwani amekuwa akimpotezea bila sababu akimtumia meseji hajibu na mengineyo.

Lakini Ben Pol aliibuka na kudai shutuma za Ebitoke kuwa anampotezea kwa kutojibu meseji zake wala kupokea simu zake sio za kweli kwani anafanya vile kwa sababu ya kazi nyingi na kwa kipindi kile alikuwa hawezi kupojea na zake kwa sababu walikuwa wanaenda mikoani kufanya Fiesta hivyo network ilikuwa mbovu ndio maana alikuwa akimpigia hampati.

Siku za hivi karibuni Ebitoke ameibuka na kudai kuwa hajawahi kuachana na Ben Pol bali kilichotokea ni kwamba aluona kama Ben Pol kama anampotezea Fulani hivi hivyo akaamua kumuweka kando na kukomaa na mishe mishe zake.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.