Ebitoke Akumbwa na Skendo Ya Kujichubua

Msanii wa maigizo Bongo Annastazia Exavery maarufu kama Ebitoke amejikuta kwenye kituo cha moto Hivi karibuni Baada ya kukumbwa na skendo ya kujichubua.

Taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinadai msanii huyo ameangaliwa sana na mashabiki zake ambao wamedai kuwa anazidi kuwa mweupe kadri siku zinvyozidi kuenda ingawa Ebitoke amekataa kabisa Skendo hizo.

download latest music    

Katika mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Ebitoke alisema weupe wake umetokana na joto kuwa kali na katika vitu ambavyo hawezi kuvifanya ni kujichubua kwa sababu anaelewa wazi kuwa kuna madhara makubwa endapo atafanya hivyo.

Najua madhara ya kujichubua siwezi kufanya hivyo kama watu wanavyonituhumu, nimebadilika na  mweupe siku hizi tofauti na zamani kwa sababu ya joto tu na siyo vinginevyo”.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.