Elizabeth Lulu aeleza kilichomvutia kwa Ally Remtullah

Mbunifu wa mavazi nchini Ally Remtullah aliandaa sherehe katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam kusherekea kutimiza miaka kumi katika kazi yake ya ubunifu wa mavazi.

Ally Remtullah anatajika sana kwa kazi yake, wasanii wengi na watu mashuhuri wamefanyiwa ubunifu na kushonewa nguo maalum na Ally Remtullah.

download latest music    
Ally Remtullah

Muigizaji wa filamu za Bongo – Elizabeth ‘Lulu’ Michael ni miongoni mwa wasanii ambao walihudhuria sherehe iliyoandaliwa na Ally Remtullah kusherekea kutimiza miaka kumi katika kazi yake ya ubunifu wa mavazi.

Akifanya mahojiano na Bongo 5 kwenye karamu hio, Lulu alisema mtaji wa shilingi elfu arobaini tu alioanza nao Ally ndo kitu kilichomvutia kwake.

“Remtullah ni mtu mwema na anayependa kazi yake, akijaribu mambo mapya huku akiyaimarisha aliyoyapata.  Kilichonivutia kwake ni kwamba mtaji alioanza nao ni mdogo sana wa shilingi elfu arobaini tu.  Hivyo nawaasa Watanzania wasikate tamaa, watumie kiasi chochote cha pesa walicho nacho ili kujilete maendeleo,” alisema Lulu.

Elizabeth ‘Lulu’ Michael

 

 

About this writer:

Martin Oduor

Ultimate keyboard ninja dedicated to bringing you the juiciest stories on blogosphere