Emmanuel Mbasha Amshukia Shilole Baada Ya Kuomba Msaada Kwa Raisi

Msanii wa nyimbo za Injili Emmanuel Mbasha amejikuta akimwagia povu zito Msanii wa Bongo fleva Zuwena Mohamed maarufu kama Shilole, baada ya kuomba msaada kwa Raisi.

Siku chache zilizopita kuna video clip iliyosambaa Kwenye mitandao ya kijamii iliyomuonyesha Shilole akimlilia Raisi Magufuli pesa kwa ajili ya kumsomesha mtoto wake.

download latest music    

Mbasha aliamua kuwatolea uvivu watu wote maarufu wanaomuandama Rais Magufuli kwa kutaka msaada wa mali ile hali wana uwezo kifedha, ikiwemo Shilole ambaye anafanya kazi za sanaa na mjasiriamali.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mbasha aliandika ujumbe huu:

 Habari za mda huu . Naandika kwa masikitiko makubwa sana juu ya watu wanaopenda kutumia vibaya huruma ya raisi wetu, haswa wasanii wa bongo movie. Jamani sera ya raisi wetu ni kila mtu afanye kazi na ndiyo maana slogan yake inasema “HAPA KAZI TU” Ukifanya kazi na kujituma kama sisi mbona maisha ni mazuri tu hapa Tanzania jamani, ila ukipenda mteremko ndiyo inaweza kuku cost ????. Dada yangu Shilole, yaani juzi tu umepost bonge la jumba hapa kila mtu akafurahia na kukupongeza hadi mie nilikupongeza, japokuwa wiki moja kabla ya hapo kuna kijana alikuwa anadai pesa zake za pili pili?.???. Leo nileshangaa kuona clip inasambaa ukilia na kuomba raisi akusaidie kukusomeshea mtoto, sitaki kukupinga ila nakuuliza na kukushauri. Jambo ambalo nakuuliza ni kwamba, Je ! Umesahau kuwa elimu ni bure kuanzia chekechea hadi form four ? Je ! Huyo unaetaka asomeshwe yuko darasa la ngapi dada yangu? Mimi nadhani vitu vingine tungevipima kabla ya kuamua kuchukua hatua. Hebu jiulize, leo raisi akikulipia ada ya mwanao unadhania hawa watoto wa maskini kabisa ambao hawana hata makazi watajisikiaje kama sio kutaka kubebeshana lawama ?

Mimi nadhani wasanii tutumie majina yetu kusaidia jamii isiyojiweza na sio kutafuta mteremko. Kweli marafiki zako wote umeshindwa hata kuwakopa kimya kimya hiyo pesa ya ada kisha uwarejeshee kidogo kidogo pale biashara inapokwenda sawa ? Mimi nadhani hichi ulichokifanya ulistahili kukifanya kwa niaba ya mtu ambaye hana jina wala connection kama zako ili utumie jina lako kumuombea msaada kwa raisi, na siyo mwanamke mpambanaji kama wewe.mie nadhani ungeandika andiko ambalo ungempelekea raisi na ukaomba akudhamini ili upate pesa Bank 400 Ml au Zaidi ukakopeshwa na ukafungua hotel kubwa na pia utakua umetengeneza ajira kwa vijana wenzetu kuliko hilo wazo,Pia kumbuka juzi tu tulikuwa na msiba kule Chato nadhani badala ya kuibuka leo na kutaka msaada angarau ungejitokeza na rambirambi kidogo ili ikuwekee mazingira mazuri ya kuja kukiwakilisha hichi kilio chako hapo baadaye. Haya ni maoni yangu kama Mtanzania huru, sitaki povu hapa jamani. Kamati yangu ya kublock kaeni mkao wa kura.kama unaweza kuzunguka na Ttcl nchi nzima.kajifunze kwa @munalove100 basi”.

Baada ya kusoma ujumbe huo Shilole alijibu kwa maneno machache tu Nakuheshimu sana kaka yangu please tulinde heshima yetu”.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.