Engine Amkingia Kifua Wolper Dhidi Ya Harmonize

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Engine amemkingia kifua aliyekuwa mpenzi wake Jacqueline Wolper dhidi ya Ex wake Harmonize baada ya sakata lao Siku mbili hizi.

Bifu la Wolper na Harmonize lilifika pabaya kiasi ya kwamba Harmonize alianika listi nzima ya wanaume ambao Wolper amebanjuka nao kitendo kilicho wakera watu wengi.

download latest music    

Engine ametumia ukurasa wake wa Instagram kumuandikia Wolper barista ya wazi huku akimuahidi kuwa hataweza kumdharau au kumchafua kamwe kwani yeye ni mshindi Kwenye macho yake.

God Never rust….My prophecy…..U will always be there because your a Winner Wolper.Nakuheshimu sana liwake jua inyeshe mvua…Katika vitu sitaweza kuja kufanya ni kumdharau mwanamke awaye yoyote maana hata kama mwanaume ni kichwa basi mwanamke ni shingo na kiwiliwili usiisahau ‘A’ kisa umeijua ‘B’ maana huwezi kuandika majina makubwa ya Kiswahili kama Mama na Baba bila kutumia A”.

Engine alikuwa Kwenye Mahusiano na Wolper na hata walitangaza kufunga ndoa na juzi Harmonize amethibitisha Mahusiano yao baada ya kumuweka Kwenye listi ya wanaume wa Wolper.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.