Enock Bella :Upendo wa Ya Moto Bado Uko Pale Pale

Moja ya wasanii ambao waliokuwa wanaunda kundi la Ya moto Band Enock Bella amefunguka na kusema kuwa watu wengiwameku wakisema kuwa kundi la ya moto band limekuwa halina mawasiliano na wamekuwa katika mgogoro tangu wametengana na kwamba hawataweza kufanya chochote pamoja lakini maneno hayo si ya kweli hata kidogo.

Enock Bella amesema  hayo alipouwa akiongea na Times Fm katika kipindi cha The Playlist  na kuongezea kuwa watu watakuja kushangaa sana pale ambapo wasanii hao watakuja kufanya   kazi tena pamoja hata kama kila mtu yuko chini ya uongozi wake.

download latest music    

Itafika sehemu tutachukua nyimbo za ya moto band na kuzipeleka tena kwa mashabiki wetu,usishangae kusikia kuna ngoma yangu na Aslay, au ukasikia ngoma yangu na beka au  moja  kati ya hao na Maromboso.bado upendo wetu uko palepale.

Baada ya Ya Moto Band kusambaratika katika umoja wa band yao wasanii hao walianza kufanya kazi kila mmoja chini ya uongozi wao huku Aslaya akiwa wa kwanza kutoa nyimbo zake na zimekuwa nyingi kuwazidi wote , huku Maromboso nae akiwa amechukuliwa na uongozi mpya wa wasafi  na kwa sasa ameanza kuachia ngoma zake.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.