Eric Shigongo: Diamond Asipoangalia Atapotezwa na Mameneja Wake

Mkurugenzi mtendaji wa Global Publishers na Mjasiriamali Eric James Shigongo amefunguka kuhusu supastaa wa muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz na kudai kuwa pamoja na kipaji chake lakini anaweza akaja kupotezwa na uongozi wake.

Shigongo aliyejipatia umaarufu kwa kichapisha vitabu na magazeti amekiri kuwa anavutiwa na Diamond kwa sababu anaona kama wote wana historia sawa ambapo wote wametokea kwenye familia au maisha ya hali duni ambapo amekiri amekua katika maisha magumu maana mama yake alikuwa anauza vitumbua lakini amekuja kujikwamua na kujitengenezea maisha mazuri kama Diamond.

download latest music    

Shigongo alifunguka hayo kwenye barua ya wazi aliyomuandikia kwenye mtandao wa Instagram siku za nyuma kidogo, ambapo aliandika:

Nampenda Diamond sana tena sana (sina uhakika kama analijua hili)  I am too proud of him ni fighter (mpiganaji) kutoka Tandale mpaka Beverly Hills with Neyo kwenye video ya wimbo wa Marry you ambao nimetoka kuuangalia    Kwenye YouTube hakika sio kitu kidogo.

Nafahamu kwa sababu niameanzia chini sana kimaisha, Nikimkumbuka Diamond tangu siku ya kwanza nilipomuona hakika nina kila sababu ya kumuita is the true sign of Tanzania.  Bila elimu kubwa bila connection bila fedha, ameweza kuvuta vizingiti vyote hadi kufika hapo alipo leo hakika ni mfano wa kuigwa kwa kila kijana wa nchi hii na duniani kote. Bravo!

Lakini nina machache ya kusema naomba wale wepesi wa kutukana wanivumilie nitoe ushauri wangu kwa Diamond kama mzazi kama kaka na Mtanzania mwenzake niseme huko anakoelekea kuna shimo asiporuka atatumbukia na huo utakuwa mwisho wake. 

Kwenye shimo hili Diamond anapelekwa na watu watatu nao ni Naseeb Abdul, Babu Tale na Salaam Sk. Nimemtaja Naseeb kwa sababu Diamond na Naseeb ni watu wawili tofauti”.

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.