Esha Buheti Adai Atampokea Mtoto Wa Nje Wa Mumewe Kwa Mikono Miwili

Muigizaji wa Bongo movie Esha Buheti ameibuka na kudai hatakuwa na tatizo endapo mume Wake Atamletea Mtoto wa nje kwani atampokea na kumlea Kama mwanaye.

Esha buheti amefunguka kuwa ameishi na mume wake kwa takribani miaka 10 sasa, hivyo hata leo hii akiamua kumletea mtoto wa nje yupo tayari kulea ila tu huyo mwanamke akae mbali na anga zake.

download latest music    

Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers Esha amefunguka na kusema haya zaidi kuhusu ishu hiyo:

Unajua mimi nimeishi na mume wangu kwa miaka 10 sasa, namjua vizuri sana, ila itakapokuja kutokea amezaa nje na akaniletea mtoto nimlee haina shida nitafanya hivyo, tena nitamlea kama mtoto wangu wa kumzaa ila tu huyo mwanamke ndio asije akasogea kwenye anga zangu kabisa”.

Kauli hiyo imeonekana kuwaacha midomo wazi mashabiki wa mwanamama huyo na wengi wao kuoenekana kupingana naye na kumshauri kutofanya hivyo kwani anakuwa kama anamruhusu mume Wake kufanya uchafu.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.