Esha Buheti Amtetea Wema Sepetu Baada Ya Kuambiwa Hastaili Kushinda Tuzo

Msanii wa Bongo movie Esha Buheti amewajia juu wasanii wote wa Bongo movie wanaodai kuwa Wema Sepetu hakustahili kushinda tuzo ya msanii bora wa kike katika tuzo za SZIFF.

Siku ya Jumapili pale Mlimani City hall Kulikuwa kuna ugawaji wa tuzo za Sinema Zetu (SZIFF) kwa wasanii wa filamu za Bongo movie na moja kati ya wasanii waliopata tuzo kubwa ni Wema Sepetu aliyejinyakulia tuzo ya msanii bora wa kike na Gabo aliyejipatia msanii bora wa kiume.

download latest music    

Kitendo cha Wema kushinda kiliibua hisia za wasanii wengi walioona Wema hajafanya movie nyingi mpaka kuweza kustahili kushinda tuzo hiyo na moja kati ya waaanii hao ni Irene Uwoya ambaye aliweka wazi kuwa Gabo alistahili tuzo ile lakini sio Wema.

Esha ameibuka na kumkingia kifua Wema na kusema hamna haja ya kumuonea wivu kwani wasanii walivyoambiwa wapeleke kazi zao kwa ajili ya kushindanishwa waligoma ila wachache waliopeleka kama Wema na Gabo wamefanikiwa kuibuka kidedea.

.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.