Esma Aelezea Anavyojiskia Mama yake Akitukanwa Mitandaoni

Mwanadada Esma Platinumz, dada wa msanii mkubwa wa bongo fleva Diamond Platinumz,ameongea na waandishi wa habari wa wasafi tv na kufunguka ya moyoni kuhusu  jinsi anavyojisikia anapoona matusi katika mitandao ya kijamii kuhusu matusi yanayomuendea mama yake mzazi.

Esma anasema kuwa mara nyingi amekuwa akikaa kimya lakini kuna muda inamuumiza sana moaka kuamua kuwajibu wanaomtukana kwa sababu hata yeye anajisikia vibaya.

download latest music    

Esma anasema kuwa pamoja na  yote lakini wanaona saa zingine hakuna cha kufanya kutokana na kuwa tayari wameshaingia katika mitandao ya kijamii na kujulikana hivyo wanavumilia hivyo hivyo  na hakuna jinsi ya kufanya kwa yanayotokea.

Najiskia vibaya sana na unajua mimi huwa sipendagi sana kuingilia katika maswala kama hayo,ila kuna wakati ukisoma unajikuta unashindwa kuvumilia hasira zako kwaio unajikuta unasoma na wewe unajibu pale pale.ila ni kitu ambacho kinauma sana lakini hakikwepeki kwa sababu tayari tulishaingia katika ulimwengu wa kujulikana, watu wanakujua na kukufatilia.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.