Esma Afunguka Sababu ya Kutohudhulia Party ya Zari S.A

Kumekuwa na maswali mengi watu wakijiuliza kuwa kwanini katika party kubwa ya familia ambayo Diamond aliifanya yeye na familia yake huko nchini Afrika ya Kusini dada yake Esma hakuwepo katka party hiyo na holidays zote ambazo familia hiyo ilisherekea nchini humo.

Ingawa kumekuwa na taarifa za chini chini kuwa hakuna maelewano mazuri kati ya Esma Platinumz na mwanamke aliyezaa na kaka yake huyo ( Zari ) kwa kipindi kirefu tangu kipindi ambacho Hamisa Mobeto  (mwanamke mwingine wa Diamond) alipojifungua ambapo dada wa msanii huyo alikuwa akionekana yupo karibu sana na Hamisa na kumuhudumia kwa kila kitu na kumfanya Zari kuchukia kitendo hicho na ndio maana wawili hao mpaka sasa hivi na kwamba Esma hajataka kwenda kwa sababu wamekuwa hawako vizuri kimahusiano.

download latest music    

Hata hivyo baada ya maneno hayo kusambaa sana ,kampuni ya habari ya GPL, iliamua kumtafuta Esma Platnumz na kumuuliza juu ya habri hizo ambazo zinasemekana kuwa zilisemwa na mtu wa karibu kabisa wa familia yao kuhusu kutoelewana kwake na wifi yake Zari na sababu ya yeye kutokuhudhuria katika party ya siku ya kuzaliwa na mtoto wa kaka yake ni kutokuelewana kwake na Zari.

Nisingeweza kuiacha biashara yangu na duka langu ambalo ni elifungua tu hivi karibuni eti niende kwenye pati,wateja wangu wasingenielewa kabisa  na ningerudi ingechukua muda mrefu kidogo kuwarejesha kwakweli.Watu wanapenda kuongea sana lakin ukweli ni kwamba mimi na Zari  hatuna tatizo lolote , kama hauamini siku nyingine akiandaa pati ntaenda tu. Alifunguka Esma Platinumz

Hata hivyo siku ya mkesha wa mwaka mpya Zari alipost video akiwa na wifi yake huyo na kusema kuwa wanavuka mwaka mpya kwa pamoja huku wakionekana na furaha.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.