Esma Aongelea Uhusiano Wake na Wema na Hamisa na Zari

Ikiwa ni kama wiki imepita tangu mtandao wa instagram kuzizima kutokana na habari za Diamond kuachwa na mama wa watoto wake wawili Zari the Bossy, dada wa Diamond, Esma Platinumz aongelea swala hilo na kukori kuwa kwa muda mrefu sasa amekuwa akikaa pembeni na kutofatilia mahusiano ya kaka yake kwa sababu hayo ni maswla yake binafsi hivyo hawezi kuyaingilia hata kidogo.

Esma anasemakuwa kwa  mahusiano ya kaka yake na mkewe yatabaki kuwa ni sehemu ya maisha yao ,na kama wanataka kuongea kitu na Diamond hatoweza kumuuliza kuhusu maswal hayo ya mapenzi zaidi ya maswala ya kifamilia tu.

download latest music    

kuna vitu vingine unawaachia wenyewe kwakweli, wao wenyewe watayaongea na kuyamaliza, hivyo havinihusu hata kidogo.hata mimi nikigombana na mtu wangu hawataingilia hayo ni ya kwao .tutakutana na kuongea maswala ya kifamilia tu hayo mengine wataongea wenyewe.

Akiongelea swala la watu latika mitandao kumuita mnafiki na kwamba amekuwa akiwafitinisha watu hasa wanawake aliowahi kutembea na kaka yake kwa kujifanya yupo kila sehemu Esma amejibu:

Mimi watu wote watu wangu, kimji chenyewe hiki kidogo unaweza kwenda sehemu ukakutana nao wote utaaacha kuongea nao, ukisema ugombane na kila aliegombana na kaka yako utakuwa mchawi wewe, mimi pia ni binadamu ninaweza nikadondoka sehemu nani ataniokota kama nitagombana na kila mtu.

Kuhusu uhusiano wake na wema esma anarudu tena na kusema hawezi kamwe kugombana na wea kwa sababu alimjua kabla ya kaka yake.hivyo hawezi kukutana na wema sehemu akamkimbia eti kwa sababu ni adui wa kaka yake.

mimi na wema ni kwa sababu tunajuana tangu zamani, siwezi kumuona sehemu alafu nikamchunia tu au nikae pembeni nisiongee nae lazima nitamfata na nitaongea nae kama ni msibani tutalia wote, pombe tutakunywa wote ,club tutacheza wote na hamisa pia ni hivyo hivyo.

Akimalizia kwa kusema pamoja na kwamba wanakuwa na mawasiliano na Diamond lakini hawezi kumuuliza chochote kuhusu kilichotokea juzi kati yake na Zari , hata kama wanaongea na mama yake mzazi lakini hawezi kufatilia kuhusu maswala ya mahusiano ya watu wengine na hata huko instagram huwa anaingia kwa ajili ya matangazo ya biashara zake tu.

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.