Esma :Wema Bado Ana Umuhimu Sana Kwangu

Mwandada anaejihusisha na mitindo kwa sasa ambae ni dada yake na msanii mkubwa nchini, Esma Platinumz amefunguka na kusema kuwa pamoja na kwamba mwanadada Wema Sepetu ameshaachana na kaka yake Diamond Platinumz yeye hawezi kuachana urafiki na Wema kwa sababu hiyo kwa kuwa bado ana umuhimu sana kwake.

Esma amesema hayo baada ya siku za hivi karibuni msanii huyo kuonekana kuwa karibu sana na familia ya diamond platinumz hata siku ya birthday ya Esma, Wema Sepetu alimtakia kheri ya kuzaliwa mwanadada huyo katika ukurasa wake wa instagram.

download latest music    

Akiongea na waandishi wa habari, Esma amesema kuwa hawezi kuwa anakosana na kila mwanamke anaeachana na kaka yake na kupatana na wale alionao katika mahusiano kwa sababu hata yeye ni mtu mzima anahitaji kuwa na marafiki hivyo hawezi kugombana na Wema.

jamani hata kidogo Wema siwezi kumuweka pembeni,hata kama aliachana na kaka yangu  lakini kwangu ana umuhimu sana.kama kila anaeachana na kaka na mimi inabidi niwe nae mbali basi inabidi nikifa nikazikwe Uganda au Afrika Kusini.

Wema na Diamond walikuwa katika mapenzi kwa muda mrefu na baadae kuachana lakini esma hakuwahi kugombana mwanadada huyo,hata hivyo kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na sekeseke linalowafanya familia ya Diamond kutofautiana na Zari the bossy ambae ni mzazi mwenzie na Diamond.

Hata hivyo huko nyuma zilishawahi kutokea tetesi kuwa kuna utofauti mkubwa wa kimahusiano kati ya Esma Platinimz na wifi yake Zari , kitu kinachomfanya hata esma kushindwa kuhudhuria sherehe nyingi ambazo kaka yake anakuwa anazifanya zilizokuwa zikimshirikisha Zari, lakini hivi karibuni esma alionekana katika sherehe ya wcb ambayo zari hakuwepo na Wema Sepetu alikuwa amearikwa.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.