Ester Kiama Aamua Kurudi Kijijini Kukimbilia Kilimo.

Mwanadada Ester Kiama kutoka bongo movies ameamua kuukacha umaarufu na usista duuh na kuamua kurudi kijijini na kujikita katika kilimo ambacho ameamini kuwa kinaweza kumtoa kuliko kitu kingine chochote kwa sasa.

Ester anasema kuwa uamuzi huo ameuamua baada ya kuona kuwa anaweza kukaa mjini sana na kupotexa muda wakati kijijini kuna shughuli nyingi za ukulima zinaweza kumuingizia kipato.

download latest music    

Ester anasema kuwa amekuwa akijaribu kufanya vitu vingi lakini anaona kabisa kuwa kila anachofanya hakimfanyi kutimiza maelngo yake hivyo kwa sasa ameona kuwa ni bora kuangukia huko kwenye kilimo tu.

kipinidi tulichonacho sasa hivi sio cha kuangalia nini cha kufanya kabisa,ni bora kujiingiza kwenye kitu chochote ambacho unaona kuwa inaweza kukiingizia kipato na kujikwamua kiamisha maana maisha ya sasa ni magumu mnoo.:-Alisema hayo alipokuwa akionea na GPL.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.