Ester kiama Hataki Wanaume Wa Mitandaoni.

Msanii wa filamu za bongo Ester Kiama amefunguka na kusema kuwa kwa upande wake wanaume wa kwenye mitandaoni ni mwiko ingawa wamekuwa wakimsumbua sana katika ukurasa wake wa instagram kwa kumtumia meseji lakini hataki kuwasikia kwa sabau wengi  ni waongo.

Ester amesema kuwa hataki kupata kashfa za kumuharibia na amekuwa akiwablock kila anapopata meseji za wanaume wanaomtaka katika mitandao hiyo.Akiongea na Ijumaa Wikienda Ester amesema kuwa wanaume hao wengi wamekuwa waongo na wanachotaka kikubwa ni kuwadhalilisha tu wasanii wa kike.

download latest music    

Nimeona kwa mastaa wengine ambao wamekuwa wakidhalilishwa na wanaume wanaowapata , hivyo sipendi kabisa yaje yanitokee na mimi kwa kweli,wanaume wengi wamekuwa wakinijaribu sana lakini wala sitaki lakini sitaki kabisa initokee.sitaki kabisa initokee kwa sababu  wanafanya hivyo kwa mastaa wa kike kwa ajili ya kuwadhalilisha  na wao wanajitangaza kuwa wanatoa na msanii fulani na hiyo ndio furaha yao.kuna wengine wanadirikimkuwapiga mpaka picha za uchi na baadae kuzivujisha.

Wasanii wengi wa kike wamekuwa wakidhalilishwa na wanaume kwenye mitandao ya kijamii kutokana na kujiingiza katika mapenzi na wanaume wanaowatongoza katika mitandao ya kijamii bila kujua wanaume hao wanakuwa na nia gani kwao.

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.