Ex Wa Ali Kiba Adai Na Yeye Anataka Kuolewa Nje Ya Nchi

Msanii wa Bongo movie aliyegeukia sanaa ya Bongo fleva Sabrina Omary ‘Sabby Angel’ ambaye pia alisemekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na staa wa Bongo fleva Ali Kiba amedai anataka kumlipizia Ex wake huyo kwa Kuolewa nje ya nchi pia.

Wiki chache zilizopita Ali Kiba alifunga ndoa na Amina Khaleef kutoka Mombasa Kenya na sasa Ex girlfriend wake Sabby Angel ameapa lazima naye aolewe na mwanaume kutoka nje ya nchi.

download latest music    

Kwenye mahojiano na Star Showbiz, Sabby Angel  amesema  siyo kwamba anaumia Kiba kufunga ndoa nje ya nchi lakini kwa mtazamo wake ameona wanaume wengi Bongo wababaishaji tu.

Yaani lazima nilipe hili, alichokifanya Kiba ni sawa lakini na mimi kama msanii naangalia hukohuko, lazima nitaolewa nje ya nchi sitaki Bongo wababaishaji wengi, wana maneno ya mdomoni tu vitendo hakuna”.

Sabby Angel ambaye hivi sasa makazi yake hapo nchini Kenya ambapo anafanya muziki ameshawahi Kuolewa mara mbili miaka ya nyuma lakini akaachika ndoa zote.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.